Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bayt (a.s) – ABNA – Mufti wa nchi ya Burundi ametembelea Ofisi ya uwakilishi wa Jamiatul Mustafa(s) katika Jiji la Dar -es- Salam, Tanzania, na kukutana na kufanya mazungumzo na Hojjatul Islam wal Muslimin, Dr. Ali Taqavi.
“Sheikh Ndikumagenge Masoud,” Mufti Mkuu wa Burundi, katika mkutano huu alisisitiza juu ya umoja wa Umma wa Kiislamu na alieleza matumaini yake kwamba kupitia mazungumzo na ushirikiano kati ya taasisi za kielimu na wanazuoni wa madhehebu mbalimbali, umoja katika Umma wa Kiislamu utaimarika.
Katika mkutano huo, mheshimiwa Mufti alipokea kwa moyo mkunjufu ushirikiano na juhudi za kuunganisha nguvu na Jamiatul Mustafa (s) katika kubadilishana fikra na maarifa ya kidini, na alieleza matumaini yake kwamba ushirikiano huu utaendelea kupanuka zaidi katika nyanja za elimu na utamaduni wa Kiislamu.
Hojjatul Islam Taqavi, Mwakilishi wa kanda wa Jamiatul Mustafa (s), katika mkutano huu, sambamba na kumkaribisha Mheshimiwa Mufti wa Burundi, alisema: Umma wa Kiislamu, kwa kufuata mafundisho ya Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w), unapaswa kusimama pamoja, na jambo hili litawezesha maadui wa dini ya Kiislamu kushindwa kuidhuru dini na maadili yake ya kidini.
Hojjatul Islam Taqavi, akisisitiza juu ya ushirikiano na kuunganisha nguvu na taasisi za kidini na kielimu, alisema: Vikao hivi ni vya thamani kubwa na vitafungua njia mpya, na moja ya malengo ya ushirikiano huu ni kueneza maarifa ya Qur’an Tukufu na kuimarisha mafundisho ya Dini Tukufu ya Kiislamu.
Aidha, Katika kikao hicho, Mwakilishi wa Jamiatul Mustafa (s) aliwasilisha ripoti ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo katika nchi za Tanzania, Burundi na Malawi, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza Elimu ya Dini Tukufu ya Kiislamu na Maarifa ya Qur'an katika eneo zima za Afrika ya Mashariki.
Mkutano huu unaonesha dhamira ya pamoja kati ya pande hizi mbili katika kukuza maadili ya Kiislamu na kuimarisha mahusiano ya kitamaduni na kidini katika maeneo ya Afrika Mashariki.
Your Comment